• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EAC yatoa tahadhari ya tishio la ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Mashariki

  (GMT+08:00) 2019-05-25 16:46:39

  Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC jana ilitoa tahadhari juu ya tishio la ugonjwa hatari wa Ebola ambao hadi sasa umeshasababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

  Kwenye taarifa iliyotolewa kwenye makao makuu yake mjini Arusha EAC imesema Ebola bado ni tishio kubwa kwa watu wa Afrika Mashariki, na kuonya kuhusu matokeo mabaya ya ugonjwa huo kwenye kilimo, utalii na maisha ya watu wa kanda hiyo. Taarifa imetilia mkazo kuwa watu wanalazimika kujiandaa vizuri kuzuia ugonjwa huo usienee hadi nje ya mipaka, ingawa hivi sasa hakuna wagonjwa wa Ebola walioripotiwa kuwepo kwenye nchi nyingine za Afrika Mashariki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako