• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • "Bolton" na wenzake wafanya mambo ya diplomasia ya Marekani kutodhibitiwa

  (GMT+08:00) 2019-05-25 20:47:43

  Profesa wa chuo cha jeshi la majini cha Marekani Tom Nichols ameandika makala inayochambua mambo ya diplomasia ya Marekani katika siku za hivi karibuni, na kusema kuwa, sera ya diplomasia ya Marekani ina dalili ya kutodhibitiwa. Na katika mambo mbalimbali ya diplomasia ya Marekani, huonekana msaidizi wa rais wa Marekani wa mambo ya usalama Bw. John Bolton.

  Kwenye uchambuzi huo Nichols anasema wanafuatiliaaliyofanya Bolton: kushinikiza wizara ya ulinzi ya Marekani kutoa mpango wa kijeshi dhidi ya Iran, kuingilia kati mambo ya ndani ya Venezuela na kulaani Russia na China bila msingi wowote.

  Ameendelea kusema kuwa Bw. Bolton akiwa mwakilishi wa watu wenye msimamo wa kutumia nguvu wa Marekani, alipokuwa mjumbe wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alisema kuwa, "Marekani inaufanya Umoja wa Mataifa ufanye kazi yake wakati inapohitaji, suala pekee kwa Marekani ni kuendana na maslahi yake ya kitaifa. Hii ndio hali halisi."

  Baada ya kuwa msaidizi wa rais wa Marekani anayeshughulikia mambo ya usalama, Bw. Bolton anaendelea kutoa uongo. Alisema makombora ya China ndio tishio kwa Russia. Kauli hiyo ilikanushwa na Russia. Mwezi uliopita, Bolton alisema jeshi la Cuba linamsaidia rais wa Venezuela kudhibiti mamlaka yake ndani ya mipaka ya Venezuela, lakini kauli hiyo ilikanushwa na waziri wa mambo ya nje wa Cuba Bruno Rodriguez.

  Ukweli ni kwamba, watu wanaodhibiti mambo ya diplomasia ya Marekani siyo Bolton pekee, bali wapo pia kina Mike Pompeo na Peter Navarro. Wana nia ya kuifanya Marekani itawale dunia. Lakini dunia ya sasa iina mabadiliko makubwa, ujeuri hauwezi kubadilisha hali ya maendeleo ya zama hii.

  Kutokana na utandawazi wa uchumi duniani , hali yenye pande nyingi ya kisiasa na mchakato wa kubadilisha mtindo wa jamii kwa njia ya teknolojia ya juu, muundo wa mamlaka ya kimataifa na uratibu wa kimataifa vimebadilika sana katika miongo mitatu iliyopita. Nchi zinazoendelea zimejitokeza, hasa nchi za soko jipya zimekuwa motisha muhimu ya ongezeko la uchumi la dunia.

  Hali halisi ya dunia kwa sasa ni kwamba, zama ya kuwepo nchi moja kubwa ya Marekani pekee imepitwa na wakati. Chini ya uchochezi wa "Bolton" na wenzake, mambo ya diplomasia ya Marekani hayatadhibitiwa, bali yataleta hatari kubwa kwa Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako