• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe maalum wa rais China ahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2019-05-26 17:56:34

  Mjumbe maalum wa rais China ambaye pia ni naibu spika wa bunge la umma la China, mwenyekiti wa kamati kuu ya chama cha CNDCA Bw. Hao Mingjin, jana tarehe 25 huko Pretoria nchini Afrika Kusini alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Afrika Kusini Bw. Cyril Rmaphosa na kufanya naye mazungumzo.

  Bw. Hao Mingjin alimfikishia rais Ramaphosa salamu za kila la heri toka kwa rais Xi Jinping , na kumkabidhi barua ya pongezi. Bw. Hao Mingjin alisema marais wa nchi hizo mbili walitembeleana mwaka 2018 na kudhihirisha mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano na urafiki wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

  Amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Afrika Kusini, na kuhimiza ushirikiano katika sekta mbalimbali kwenye kiwango cha juu zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako