• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza umuhimu wa kupunguza kodi na ada kwenye kutoa huduma nzuri za fedha

  (GMT+08:00) 2019-05-26 17:58:06

  Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza umuhimu wa kupunguza kodi na ada mbali mbali na kuboresha huduma za fedha, ili kupunguza mzigo kwa makampuni na kuhimiza maendeleo.

  Bw. Li ametoa kauli hiyo akiwa ziarani mkoani Shandong, na kusema kupunguza kodi na ada mbalimbali ni muhimu, kwa kuwa kunasaidia kuendana na hali ya sasa ya kupungua kwa ongezeko la uchumi na kunaweza kuwa na manufaa kwa muda mrefu.

  Bw. Li amesema kutokana na China kuwa na soko kubwa linalopanuka, makampuni mbalimbali yakitumia uvumbuzi wa kiteknolojia, na kufanya juhudi zao na kushirikiana kwa mapana, yanaweza kudhibiti soko na kupata imani ya wateja.

  Bw. Li pia amesema serikali itaendelea kuboresha sera na kuhimiza makampuni kuwekeza zaidi kwenye utafiti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako