• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hisia za kutaka kudhuriwa zaathiri msingi wa uhusiano kati ya China na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-05-26 18:01:14

  Mkuu wa chuo kikuu cha Yale cha Marekani Bw. Peter Salovey hivi karibuni ameandika barua ya wazi akieleza wasiwasi kuhusu uhusiano kati ya Marekani na China, na kuongezeka kwa ukaguzi wa mawasiliano ya kitaaluma, na kusisitiza kuwa kufungua mlango ni kiini cha mafanikio ya vyuo vikuu vya Marekani, pia ni alama ya chuo kikuu cha Yale katika siku zote.

  Barua hiyo inaonyesha kuwa mawasiliano ya watu ambayo ni moja ya misingi ya uhusiano kati ya China na Marekani, yanakabiliwa na tishio la "hisia za kutaka kudhuriwa" la baadhi ya wamarekani. Baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanadai hali ya uwepo upande mmoja na kujilinda kibiashara, wanaichukulia China kama adui ya Marekani, na kuilaani China kuvamia kiuchumi na kushutumu wanafunzi wa China wanaosoma nchini Marekani kuwa ni wapelelezi.

  Mawasiliano ya kirafiki kati ya watu na watu ni chanzo cha uhusiano kati ya nchi na nchi, na msingi wa maendeleo uhusiano kati ya China na Marekani umepatikana na mawasiliano ya watu katika sekta mbalimbali. Kila siku watu zaidi elfu 14 wanakwenda na kurudi kati ya China na Marekani, na watu zaidi milioni 5.3 wamesafiri kati ya China na Marekani. Mambo hayo yameshuhudia ustawi na karibu wa mawasiliano ya watu kati ya China na Marekani.

  Lakini baadhi ya wanasiasa wa Marekani wana hisia za kutaka kudhuriwa wanayachukulia mawasiliano ya watu kati ya China na Marekani kwa mambo ya hisia za kutaka kudhuriwa. Wanataka kufunga mlango wa mawasiliano ya watu kati ya nchi hizo mbili. Mkurugenzi wa FBI ya Marekani Bw. Christopher Wray amesema, China imekuwa tishio kwa jamii yote ya Marekani, inahitaji jamii yote kuitikia. Kauli hiyo isiyo na msingi inawataka watu wa Marekani wawe hofu kuhusu China, ili kuunga mkono vitendo vyao.

  Ukweli ni kwamba, hisia hizo za kutaka kudhuriwa haziwezi kudanganya watu wenye akili. Takwimu zinaonyesha kuwa, katika miaka 9 iliyopita China ni nchi iliyotoa wanafunzi wengi zaidi wanaosoma nchini Marekani. Profesa msaidizi wa chuo kikuu cha Massachusetts cha Marekani Bw. Paul Musgrave amesema soko nzuri la vyuo vya Marekani ni China, Marekani inaweka vikwazo dhidi ya wanafunzi wa China kwa upande mmoja, kutaleta hatari kwa vyuo vikuu vya Marekani, hasa mfumo wa elimu ya juu wa Marekani hautadumishwa.

  Mawasiliano ya kina kati ya watu wa China na Marekani yataendelezwa na bila kuzuiliwa. Hisia za kutaka kudhuriwa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa Marekani, kamwe haziwezi kutokomeza mawasiliano ya watu wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako