• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yapitisha itifaki ya kuzuia na kudhibiti hatari za kiusalama

    (GMT+08:00) 2019-05-27 09:32:46

    Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) limeridhia itifaki ya kikanda ili kuzuia na kudhibiti hatari za kiusalama katika kanda hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, itifaki ya kuanzisha Idara ya diplomasia na upatanisho itatumika kama mwongozo mkuu kwa nchi wanachama katika kuchukua hatua za uingiliaji kwa ufanisi na uwazi, kupeleka wajumbe au wasuluhishi, na kushiriki kwa kiasi kikubwa katika kuzuia, kudhibiti na kutatua migogoro katika kanda hiyo.

    Chini ya jukwaa la Kamati ya mabalozi, wawakilishi kutoka nchi wanachama wa IGAD pia wameidhinisha Kitengo cha Upatanishi cha IGAD kuanzisha taratibu zinazolenga kuimarisha na kuongeza uwezo wa upatanishi wa nchi za Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako