• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kushinda vikwao vya Marekani kwa moyo wa "safari ndefu"

  (GMT+08:00) 2019-05-27 16:48:50

  Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alipofanya ukaguzi mkoani Jiangxi, aliweka maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya safari ndefu ya Jeshi Jekundu la China, na kusisitiza kuwa moyo wa "safari ndefu" utang'aa daima.

  Ili kuepuka mashambulizi ya jeshi la Kuomindang, mwezi Oktoba mwaka 1934, Jeshi Jekundu chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China lilifanya safari ndefu ya kilomita elfu 12.5. Jambo hili linachukuliwa kama moja ya mambo yaliyoathiri zaidi mustakabali wa dunia katika karne iliyopita. Hivi leo, ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa kiuchumi, China inawahamasisha wananchi wake kujitahidi kwa ajili ya ustawi wa taifa kwa moyo wa "safari ndefu", na hii ni hatua yenye maana kubwa.

  Hivi karibuni Marekani imeongeza vikwazo dhidi ya China, haswa katika sekta ya sayansi na teknolojia ya juu, huku ikihimiza au kulazimisha nchi nyingi kuisaidia kuzuia maendeleo ya China. Alhamisi iliyopita waziri wa mambo ya nje ya Marekani Mike Pompeo alisema anakutana na viongozi wa nchi mbalimbali ili kufafanua "hatari ya Kampuni ya Huawei ya China". Takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Habari za Viwanda ya China zinaonesha kuwa, hadi tarehe 17 mwezi huu, zaidi ya makampuni 260 ya China yamewekwa na Marekani katika orodha nyeusi, na kuchukua nafasi ya pili duniani baada ya Russia.

  Madhumuni ya Marekani kuwekea China vikwazo ni kuishinikiza China kukubali makubaliano yasiyo na haki ya kibiashara. Lakini ukweli ni kwamba, Marekani inajigamba na kudharau uwezo wa China. Wachina siku zote wanajihamasisha kwa moyo wa "safari ndefu", na kuzingatia zaidi maslahi ya taifa. Kutokana na changamoto za nje, watashirikiana vizuri na kufanya juhudi kadiri wawezavyo mpaka kupata ushindi wa mwisho.

  Kujipatia maendeleo ya sayansi na teknolojia si haki ya nchi fulani, bali ni matumaini ya pamoja ya binadamu. Kwa kukabiliwa na vikwazo vya Marekani, China haitarudi nyuma, bali itaendelea kuendeleza sayansi na teknolojia, ili kunufaisha wananchi wake na binadamu wote.

  Wakati huohuo, China itaendelea kuunga mkono makampuni yake ikiwemo Huawei kuimarisha ushirikiano na nchi za nje, na kulinda haki na maslahi halali ya makampuni ya nchi za nje ikiwemo Marekani.

  Moyo wa "safari ndefu" si kama tu ni nguvu ya kiroho ya wachina, bali pia ni mali ya kiroho ya binadamu wote. Mwandishi wa habari wa Marekani Bw. Harrison Evans Salisbury alisema, moyo huo ulisisimua watu wengi zamani, na sasa bado unaheshimiwa na watu wa nchi mbalimbali duniani, na utakuwa mnara mkubwa wa ushujaa wa binadamu.

  Kizazi tofauti cha wachina wana safari ndefu tofauti, na kila kizazi wana imani ya kushinda matatizo yote yanayowakabili kwa moyo wa "safari ndefu".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako