• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burkina Faso yathamini uhusiano wa kirafiki kati yake na China uliopotea

    (GMT+08:00) 2019-05-27 18:51:57

    Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Bw. Alpha Barry amesema Burkina Faso itaendelea kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuthamini uhusiano wa kirafiki kati yake na China uliopotea.

    Ubalozi wa China nchini Burkina Faso tarehe 26 huko Ouagadougou uliandaa tafrija ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu nchi hizo zirudishe uhusiano wa kibalozi, na maonesho ya picha za matokeo ya kurudisha uhusiano huo. Bw. Barry alipohudhuria tafrija hiyo alisema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio makubwa tangu urudishwe mwaka mmoja uliopita.

    Ameseam China inazingatia na kufuatilia matarajio ya Burkina Faso na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo na usalama na amani ya eneo hilo. Amesema kurudisha uhusiano wa kibalozi kwa pande hizo mbili kulifuata mwelekeo wa kipindi hiki, na kulingana na maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizo mbili. Pia amesema Burkina Faso itafanya juhudi na China kuhimiza ushirikiano wa pande hizo mbili upate mafanikio mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako