• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwango cha afya ya wanawake na watoto wa China chainuka

    (GMT+08:00) 2019-05-27 19:45:47

    Kamati ya afya na usafi ya China leo imetoa ripoti ya mwaka 2019 ya maendeleo ya mambo ya afya ya wanawake na watoto wa China.

    Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, tangu China mpya ianzishwe miaka 70 iliyopita, kiwango cha afya ya wanawake na watoto kimeinuka, kiasi cha vifo cha wajawazito katika mwaka 2018 kimepungua hadi kufikia watu 18.3 ya laki moja, kiasi cha vifo vya watoto kimepungua hadi kufikia watoto 6.1 ya elfu moja, wastani wa maisha ya watu wa China umefikia miaka 77, ambao ni mrefu kuliko kiwango cha wastani cha nchi zenye mapato ya kati na ya juu.

    Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imekuwa inatilia maanani suala la afya ya wanawake na watoto, na kutoa kipaumbele kwa suala hilo. China imefanya juhudi kutoa huduma za kimfumo na mfululizo za afya ya wanawake na watoto, na kupunguza tofauti kati ya miji na vijiji, na tofauti kati ya maeneo tofauti.

    Mkurugenzi wa idara ya afya ya wanawake na watoto katika kamati hiyo Bw. Qin Geng, amesema mpango wa chanjo kwa watoto wa China umepata ufanisi, kiasi cha watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 wanaoishi na virusi vya hepatitis B kimedhibitiwa na kuwa chini ya asilimia moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako