• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japan na Marekani zapanga kuharakisha mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara

    (GMT+08:00) 2019-05-27 19:55:39

    Viongozi wa Japan na Marekani wamesema wanakubaliana katika mambo mengi muhimu baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Tokyo.

    Wakiongea kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe amesema nchi hizo mbili zitaharakisha mazungumzo yaliyoanza mwezi April kuelekea kufikia kwenye makubaliano ya biashara.

    Japan imekuwa ikitaka ushuru dhidi ya bidhaa zake za viwanda zinazouzwa Marekani uondolewe, hasa kwenye magari, sababu iliyoifanya Marekani ijitoe kwenye makubaliano ya biashara ya nchi za Pasifi (TPP).

    Marekani nayo inataka kupata soko nyeti la kilimo la Japan, la nyama, ngano na nyama ya nguruwe.

    Viongozi hao pia wamesema wanakubaliana kabisa kuhusu suala la Penisula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako