• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mutharika ashinda uchaguzi urais Malawi

    (GMT+08:00) 2019-05-28 08:42:18

    Rais wa sasa wa Malawi Peter Mutharika ametangazwa kushinda kwenye uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali, huku vyama vya upinzani vikidai kuwa kulikuwa na vitendo vya uvunjifu wa sheria katika uchaguzi huo.

    Mutharika amepata asilimia 38.57 ya kura na kumshinda mpinzani wake Lazarus Chakwera, ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Malawi Congress Party (MCP) aliyepata asilimia 35.41 ya kura, huku mpinzani wake mwingine Bw. Saulos Chilima ambaye ni makamu wa rais akipata asilimia 20.24 ya kura.

    Wakati huo huo, uchaguzi wa bunge pia ulifanyika ambapo chama tawala Democratic Progressive Party (DPP) kimepata viti 62 kati ya 193, chama kikuu cha upinzani kimepata viti 55, na wengine wasio na vyama wamepata viti 55.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako