• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • LANGALANGA (F1): Vettel aionya timu ya Ferrari wakati Hamilton akishinda mbio za Monaco

  (GMT+08:00) 2019-05-28 10:31:53

  Dereva wa kampuni Ferrari, Sebastian Vettel ameionya timu yake kuwa wanayo kazi kubwa ya kufanya mbele yao baada ya kushuhudia kwa mara nyingine wakimaliza katika nafasi ya pili kwenye mbio za Monaco.

  Akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mbio hizo ambazo zilishuhudia ushindani mkali, bingwa huyo mara nne wa mashindano ya langalanga, ameeleza kuridhishwa na nafasi aliyomaliza.

  Mbio za Monaco zilishuhudia dereva wa kampuni wa Mercedes, Lewis Hamilton akimaliza katika nafasi ya kwanza licha ya kuwa alitumia matairi ambayo yalihatarisha nafasi yake.

  Baada ya ushindi, Hamilton amesema ushindi wake ni zawadi kwa mkongwe wa mbio hizo aliyefariki juma lililopita Niki Lauda ambaye alikuwa akifanya kazi na Mercedes na alikuwa na ushawishi mkubwa kwa Hamilton.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako