• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Zamalek bingwa kombe la Shirikisho barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-05-28 10:33:10

    Penalti za viwango vya juu zilizopigwa na wachezaji wa klabu ya Zamalek ya Misri zilitosha kuipa ubingwa timu hiyo na kufanikiwa kumaliza ukame wa kutwaa taji kubwa barani Afrika uliodumu kwa karibu miaka 16, ambapo imefanikiwa kutwaa kombe la shirikisho barani Afrika.

    Huku kukiwa hakuna sheria ya muda wa nyongeza katika michuano inayosimamiwa na CAF, timu hizo zililazimika kupigiana matuta ambapo Zamalek ilipata penati zote 5 huku Berkane ikipata mabao 3.

    Kocha wa Zamalek ambaye aliwahi kukipiga na klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza Christian Gross raia wa Sweden, anakuwa kocha wa pili kutoka kwenye taifa hilo kushinda taji la shirikisho kama alivyowahi kufanya mwenzake Michel Decastel mwaka 2007 akiwa na klabu ya Tunisia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako