• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Uwekezaji binafsi ni muhimu katika kufikia malengo ya taifa ya umeme

    (GMT+08:00) 2019-05-28 19:43:06

    Wataalamu wanasema malengo ya Rwanda ya upatikanaji wa umeme kwa wote kufikia mwaka 2024,kama yalivyoelezwa katika mkakati wa kitaifa wa mabadiliko (NST1) yanaweza kufikiwa kama uwekezaji katika sekta binafsi utaimarishwa.

    Hata hivyo,uwekezaji mdogo katika sekta ya nishati huenda ukaathiri malengo hayo.

    Kufikia sasa,upatikanaji wa umeme unasimama katika asilimia 51 kutoka asilimia 9 mwaka 2010,ambapo kati yazo,asilimia 38 ziko katika gridi inayosambazwa na serikali,kupitia kampuni ya Rwanda Energy Group na asilimia 13 zinachangwa na wawekezaji binafsi katika miaka minne iliyopita.

    Ili kuhakikisha upatikanaji umeme kwa wote kufikia mwaka 2024,serikali inalenga kusambaza umeme kwa asilimia 52 ya ya jumla ya idadi ya watu,kwa kutumia vituo vyake vilivyoko kwenye gridi ya taifa,wakati uwekezaji usio kwenye gridi unatarajiwa kuchangia asilimia 48 kupitia umeme wa jua au gridi ndogo.

    Fauka ya hayo takwimu zinaonyesha kuwa sekta binafsi haijajitolea sana kuwekeza katika sekta ya nishati kwa sababu serikali inatarajia wawekezaji binafsi kuchangia asilimia 48 ya jumla ya umeme kufikia mwaka 2024.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako