• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mitaji ya kimataifa yapiga kura ya ndiyo kwa uchumi wa China

  (GMT+08:00) 2019-05-28 19:51:03

  Shirika la Morgan Stanley Capital International Index leo limeinua kiwango cha nafasi ya soko la hisa la China kwenye alama yake ya kimataifa ya hisa. Hii ni mara nyingine kwa mitaji ya kimataifa kupiga kura ya ndiyo kwa maendeleo ya uchumi wa China.

  Kutokana na ongezeko la hatua za upande mmoja na mivutano ya kibiashara duniani, mashirika mbalimbali ya kimataifa yamepunguza makadirio yao kuhusu ukuaji wa uchumi wa dunia. Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa, kasi ya maendeleo ya uchumi wa dunia kwa mwaka huu itapungua na kuwa asilimia 2.7 kutoka 3, na ongezeko la biashara ya kimataifa pia litapungua na kuwa asilimia 2.7 kutoka 3.4 ya mwaka jana. Licha ya umoja huo, Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa pia zimepunguza makadirio yao kuhusu maendeleo ya uchumi wa dunia.

  Hata hivyo, ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa kiuchumi, nchi ya kwanza kwa mauzo ya bidhaa na nchi ya pili kwa maagizo ya bidhaa, China imedumisha mwekeleo mzuri wa maendeleo ya uchumi.

  Mwaka jana, pato la taifa GDP la China lilizidi dola trilioni 13.6 za kimarekani, na China imechangia asilimia 30 ya maendeleo ya uchumi wa dunia. Mwaka huu, licha ya kukabiliwa na vita vya kibiashara vinavyochochewa na Marekani, China imedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi, na kuendelea kuwa injini ya uchumi wa dunia.

  Kati ya makampuni yanayoathiriwa na hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru wa bidhaa kutoka China, karibu nusu ni ya nchi za nje ikiwemo Marekani. Kampuni ya Novelis ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kuwa itaongeza uwekezaji wa dola milioni 180 za kimarekani nchini China bila kujali mivutano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

  Si Kampuni ya Novelis pekee, makampuni mengi ya Marekani nchini China yanaona kuwa uchumi wa China utaendelea vizuri, na China ina uwezo wa kufanya mambo yake vizuri. Katikati ya mwezi huu, Shirikisho la Wafanyabiashara wa Marekani nchini China lilifanya hojaji kwa makampuni karibu 250 ya Marekani nchini China, na hojaji hiyo inaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya makampuni hayo yameathiriwa na hatua ya ongezeko la ushuru iliyofanywa na serikali ya Marekani, lakini yatazingatia zaidi soko la China.

  Sababu ya mashirika, viongozi na makampuni ya nchi za nje kuwa na imani kuhusu China ni kwamba, China ina miundombinu bora, mfumo kamili wa sekta za viwanda, mazingira mazuri ya kibiashara, soko kubwa la matumizi, na moyo wa kufanya kazi kwa bidii wa wachina. Kwa kushirikiana na dunia nzima, China itaanzisha mustakabali mzuri zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako