• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkoa wa Hebei wapata maendeleo makubwa katika miaka 70 iliyopita

  (GMT+08:00) 2019-05-28 20:54:20

  Katibu mkuu wa kamati ya chama cha kikomunisti cha China mkoani Hebei, Bw. Wang Dongfeng, leo amesema tangu China mpya kuanzishwa miaka 70 iliyopita, mkoa wa Hebei umepata maendeleo makubwa katika mambo mbalimbali. Thamani ya jumla ya uzalishaji wa mali ya mkoa huo kwa mwaka jana iliongezeka mara 800 kuliko ilivyokuwa mwanzoni mwa kuanzishwa kwa China mpya.

  Amesema maisha ya watu wa mkoa huo yameboreshwa, mapato ya watu wa mijini na vijijini kwa mwaka 2018 yameongezeka kwa mara 119.5 na mara 123 mtawalia kuliko mwaka 1978.

  Bw. Wang Dongfeng pia amefafanua matokeo yaliyopatikana kwa sasa ya mambo matatu yanayofanywa na mkoani Hebei, yaani maendeleo shirikishi ya Beijing, Tianjin na Hebei, ujenzi wa eneo jipya la Xiong'an, na michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako