• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele kuhusu Ushirikishaji wa kifedha wa kidijitali kati ya China na Afrika wafunguliwa Nairobi

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:04:13

    Watunga sera za kifedha na wataalamu kutoka taasisi na mashirika ya China na Afrika wamekutana mjini Nairobi, Kenya, kujadili jinsi ya kuharakisha uwekezaji na ushirikiano kwa ajili ya ushirikishaji wa kifedha barani Afrika.

    Katika Mkutano wa Kilele wa mwaka 2019 Kuhusu Ushirikishaji wa kifedha wa kidijitali kati ya China na Afrika, wataalamu wamejadili jinsi ya kuhimiza ajenda ya maendeleo ya Ushirikishaji wa kifedha wa kidijitali DFI kupitia ujenzi wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika, ili kurahisisha mabadilishano ya ujuzi, ushirikiano na uwekezaji.

    Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, mkuu wa Chuo cha Ushirikishaji wa Kifedha cha China CAFI Bei Douguang, amesema mkutano huo utaanzisha jukwaa kwa ajili ya mazungumzo, mawasiliano na ushirikiano, na ushirikishaji wa kifedha katika nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja, na utatoa fedha kwa mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati, ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako