• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wananchi wa China hawafurahi kuona madini ya udongo adimu yanayouzwa nje kutumiwa kuzuia maendeleo ya China

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:04:45

    Ofisa wa Tume ya Maendeleo na Mageuzi ya China NDRC amesema, China, ikiwa ni nchi inayotoa madini ya udongo adimu kwa wingi duniani, siku zote inafuata mkakati wa maendeleo ya sekta hiyo unaosisitiza uwazi, uratibu na kushirikishana, lakini wananchi wake hawatafurahi kuona madini ya udongo adimu yaliyouzwa nje yanatumiwa kuzuia maendeleo ya China.

    Ofisa huyo amesema, katika zama za utandawazi, maendeleo hayapatikani bila kuwa na ushirkiano, na kwenye maendeleo ya sekta ya udongo adimu, China inashikilia kanuni ambayo raslimali za udongo huo zinatakiwa kutoa kipaumbele kukidhi kwanza mahitaji ya ndani, na China pia inapenda kukidhi mahitaji halali ya nchi mbalimbali duniani kwa madini hiyo.

    Akizungumzia mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, ofisa huyo amesisitiza kuwa hakuna mshindi kwenye vita ya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako