• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yafuatilia hali ya kibinadamu nchini Syria

  (GMT+08:00) 2019-05-29 09:07:08

  Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ma Zhaoxu amesema China inafuatilia sana hali ya kibinadamu nchini Syria na kuitaka jumuiya ya kimataifa itafute ufumbuzi wa msukosuko wa nchi hiyo. Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama, Balozi Ma amesema China inaunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Umoja wa Mataifa na wadau husika katika kuboresha hali ya kibinadamu nchini Syria. Ameongeza kuwa suala la Idlib limesababishwa na magaidi wanaodhibiti eneo hilo na kusisitiza umuhimu wa kuweka uwiano katika vita dhidi ya makundi yote ya kigaidi yaliyoorodheshwa na Baraza la Usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako