• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 23 wauawa katika shambulizi lililotokea nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:43:21

    Msemaji wa polisi wa Jimbo la Zamfara la Nigeria Bw. Mohammed Shehu amesema, wanakijiji 23 wameuawa na watu wenye silaha jana, kwenye jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

    Bw. Shehu amesema vijiji vya Tunga na Kabaje vilivyoko kwenye eneo la Kaura-Namoda jimboni hilo vimeathiriwa vibaya na shambulizi hilo.

    Mamlaka ya jimbo hilo imethibitisha kuwa zaidi ya watu 100 wenye silaha walivamia vijiji hivyo viwili wakati wakazi wa vijiji hivyo walipokuwa wakielekea mashambani.

    Chanzo cha shambulizi bado hakijajulikana, na hakuna kundi lenye silaha lililotangaza kuwajibika na shambulizi hilo.

    Habari nyingine zinasema, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafuatilia vurugu zilizotokea kaskazini magharibi nchini Nigeria zilizowafanya watu 20,000 kukimbilia nchi jirani ya Niger tokea mwezi Aprili, na kusema linashirikiana na serikali ya Niger kutoa msaada wa lazima na kuwaandikisha wakimbizi wapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako