• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zimbabwe yalaani ongezeko jipya la bei ya mafuta

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:58:27

    Baraza la mawaziri la Zimbabwe limekosoa duru mpya ya ongezeko la bei ya mafuta, huku likionya kuwa idara za usimamizi zitafanya juhudi zote kutekeleza sheria.

    Baadhi ya vituo vya mafuta jana viliongeza bei ya mafuta kutoka dola 5 hivi za RTGS hadi kufikia dola 7 za RTGS kwa lita. Ongezeko hilo linakuja wiki moja baada ya idara ya usimamizi wa nishati ya nchi hiyo ZERA kupandisha bei ya mafuta kutoka dola 3.35 za RTGS kwa lita hadi dola 4.97 za RTGS jumatatu iliyopita.

    Wakati bei ya mafuta inaendelea kuongezeka, bidhaa hiyo bado iko katika hali ya upungufu kutokana na nchi hiyo kukabiliana na ukosefu wa akiba ya fedha za kigeni ili kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako