• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Simba shangwe kama lote, yakabidhiwa kombe, Kagera Sugar na African Lyon zashuka daraja.

  (GMT+08:00) 2019-05-29 10:36:52

  Sasa yametimia, wakati Simba ikiandaliwa mapokezi makubwa jijini Dar es Salaam wakiwa na kombe la ubingwa, Kagera Sugar na African Lyon zimeungana kuaga ligi kuu Tanzania bara na kushuka daraja kucheza ligi daraja la kwanza msimu uajo.

  Kagera Sugar imeshuka daraja baada ya kukubali sare ya 1-1 na Mbao FC, African Lyon yenyewe imeshuka daraja baada ya kuburuza mkia katika ligi hiyo.

  Wakati huo huo, wachezaji wa kigeni waliotikisa ligi hiyo ni Meddie Kagere na Haruna Niyonzima wa Rwanda, Emmanuel Okwi wa Uganda wanaokipiga katika klabu ya Simba, Heritier Makambo wa DRC anayechezea Yanga, na Donald Ngoma anayekipiga Azam FC, wameweza kuzisaidia timu zao kupata matokeo chanya na kuonyesha vipaji vyao vya ziada wawapo uwanjani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako