• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mahakama Sierra Leone yafuta mashtaka ya rushwa dhidi ya rais wa chama cha soka Isha Johansen

    (GMT+08:00) 2019-05-29 10:37:46

    Rais wa chama cha soka nchini Sierra Leone, Isha Johansen amefutiwa mashtaka yote ya rushwa dhidi yake na mahakama ya mjini Freetown.

    Kufutiwa mashtaka kwa Johansen sambamba na katibu mkuu wake Christopher Kamara, kunatoa nafasi ya nchi hiyo kuondolewa adhabu iliyokuwa imewekwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

    FIFA iliifungia Sierra Leone mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na Serikali kuingilia shughuli za mpira kwa kuwaondoa madarakani Johansen na wenzake na kuwa inasubiri kwanza kumalizika kwa kesi dhidi ya Johansen kabla ya kuchukua hatua nyingine ikiwemo kuondoa adhabu iliyowekewa.

    Mashtaka hayo yalisababisha nchi hiyo kukosa nafasi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako