• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wajumbe wa makampuni 500 makubwa zaidi duniani wajadili ushirikiano wa biashara ya huduma

  (GMT+08:00) 2019-05-29 16:49:35

  Mkutano wa kilele wa makampuni 500 makubwa zaidi duniani umefanyika jana hapa Beijing. Wajumbe kutoka makampuni ya nje wanaona kuwa, China ina nafasi kubwa ya kuendeleza biashara ya huduma, kwani serikali ya nchi hiyo inaendeleza sera ya kufungua mlango kwa nia thabiti.

  Wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wenye kauli mbiu ya "kufungua mlango na uvumbuzi, kuongoza maendeleo mapya ya biashara ya kimataifa ya huduma" wanaona kuwa, China imedumisha utulivu wa maendeleo ya uchumi. Mtendaji mkuu wa tawi la Kampuni ya Uhasibu ya Deloitte nchini China, Bw. Zeng Shunfu anasema,

  "Tunaona kuwa China ina nafasi kubwa ya kuendeleza biashara ya huduma. Tunakubali kuwa China inatakiwa kuharakisha kufungua mlango katika sekta kadhaa ikiwemo, fedha, mawasiliano ya barabara, elimu na afya."

  Katika miaka ya hivi karibuni, biashara ya huduma ya China imeendelea kwa kasi kubwa. Mwaka jana, thamani ya biashara ya huduma kati ya China na nchi za nje ilifikia karibu dola bilioni 740 za kimarekani, na kushika nafasi ya pili duniani.

  Hata hivyo ikilinganishwa na biashara ya bidhaa ambayo ilizidi dola bilioni 4.35 za kimarekani kwa mwaka jana, China ina nafasi kubwa ya kuendeleza biashara ya huduma. Naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa maendeleo ya Baraza la Serikali la China Bw. Ma Jiantang amesema, China inafungua mlango zaidi kwa nje katika sekta ya huduma. Anasema,

  "Tunapofungua mlango katika sekta ya huduma, tutaweka kipaumbele katika uhakikisho wa sera. Tutakamilisha mfumo wa usimamizi wa forodha na njia ya huduma, na kuinua kiwango cha miundombinu na kurahisisha biashara ya huduma."

  Bw. Ma ameongeza kuwa, China itajaribu teknolojia za habari na dijitali, kuendeleza biashara ya huduma mpya. Baadhi ya wajumbe wanatarajia kuwa China itaharakisha kuboresha mazingira ya biashara na huduma. Naibu mkuu wa tawi la kampuni ya Magari ya Daimler AG nchini China Bw. Leng Yan anasema,

  "Tuna imani kubwa kwa huduma za serikali ya Beijing. Katika miaka ya hivi karibuni, mji wa Beijing umetoa hatua mpya mbalimbali, kwa mfano umeongeza muda wa kuagiza magari ya kutathmini kuwa miezi 24 kutoka miezi 6."

  Aidha, sheria ya uwekezaji wa nje itakayoanza kutekelezwa tarehe Mosi Januari mwakani itatoa uhakikisho mpya wa sheria kwa wawekezaji kutoka nchi za nje, na kuanzisha mazingira mazuri kwa maendeleo ya biashara ikiwemo biashara ya huduma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako