• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai Marekani itaheshimu kanuni ya soko, na kutoingiza mambo ya siasa kwenye suala la ubadilishaji wa fedha

    (GMT+08:00) 2019-05-29 19:11:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, uamuzi wa wizara ya fedha ya Marekani kusema China haiendeshi kiwango cha ubadilishaji wa fedha, unaendana na ujuzi wa kimsingi na maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

    Pia amesisitiza kuwa China inatumai Marekani itafuata utaratibu wa kimataifa, kuheshimu kanuni ya soko, na kutoingiza siasa kwenye suala la ubadilishaji wa fedha.

    Bw. Lu Kang amesema, China itaendelea kufanya mageuzi ya soko la ubadilishaji wa fedha kwa kina, na kuendelea kuboresha utaratibu wa ubadilishaji wa kiwango cha fedha kwa msingi wa mahitaji ya fedha sokoni, ili kudumisha utulivu wa kiwango kinachofaa na chenye uwiano cha ubadilishaji wa Renmnbi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako