• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani haipaswi kuwa na wasiwasi kwamba China itachukua nafasi yake

  (GMT+08:00) 2019-05-29 19:52:18

  Baadhi ya wanasiasa wa Marekani hivi karibuni wamesema, uchumi wa China unakua kwa haraka, na China itakuwa na nguvu kubwa zaidi kuliko Marekani. Lakini ukweli ni kwamba, China haiwezi kuchukua nafasi ya Marekani kuwa lengo lake la maendeleo.

  Baada ya vita baridi, Marekani imedumisha kithabiti hadhi yake ya "superpower" pekee duniani. Hadi sasa Marekani bado iko mbele duniani katika nguvu za kiuchumi, kifedha, kijeshi na kisayansi. Hata hivyo, baadhi ya wamarekani wana wasiwasi kuwa huenda nchi nyingine itashinda Marekani.

  Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, uwezo wa uchumi na sayansi wa China umepata maendeleo makubwa, na pengo kati yake na Marekani limepungua kwa kiasi kikubwa, lakini pengo hilo bado ni kubwa. Mwaka 2017, serikali ya Marekani kwa mara ya kwanza ilichukulia China kama mshindani wake mkuu. Hivi karibuni, Marekani imeongeza hatua za kuzuia maendeleo ya China, ikiwemo kuongeza ushuru kwa bidhaa za China, na vikwazo dhidi ya makampuni ya teknolojia ya China. Kwani inaona kuwa China inajaribu kuchukua nafasi yake duniani kufuatia maendeleo ya kasi ya kiuchumi na teknolojia.

  Lakini kazi kuu ya China ya hivi leo ni kuboresha maisha ya watu wake, na kufanya vizuri mambo mengine ya ndani. China haina mawazo ya umwamba, na China yenye nguvu itakuwa na manufaa kwa dunia nzima na kuleta fursa kubwa ya maendeleo kwa nchi nyingine. Kama China na Marekani zikishindwa kutatua mvutano wa kibiashara, si kama tu maslahi ya nchi hizo mbili yatadhuriwa, bali pia maslahi ya dunia nzima yataathiriwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako