• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka jamii ya kimataifa kusaidia Afrika kutumia maliasili zake

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:06:21

    Mjumbe wa China ameitaka jamii ya kimataifa kuisaidia Afrika kutumia vizuri fursa ya maliasili zake na kuzuia matumizi mabaya na biashara haramu.

    Mshauri na mratibu wa masuala ya kisiasa wa China kwenye ujumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, Yao Shaojun amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kusaidia nchi husika katika kuanzisha na kuboresha mifumo ya utawala ikiwemo mahakama, matumizi ya sheria, na uongozi katika matumizi ya maliasili hizo, pia kuongeza juhudi katika kupambana na matumizi mabaya na usafirishaji haramu wa rasilimali hizo.

    Yao ameutaka Umoja wa Mataifa kuimarisha zaidi ushirikiano na Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kikanda barani Afrika katika usimamizi wa maliasili, na kupambana na matumizi mabaya pamoja na usafirishaji haramu wa maliasili hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako