• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo kati ya Liu Xin kutoa CGTN na Trish Regen kutoka Fox News yafanyika

    (GMT+08:00) 2019-05-30 11:59:05

    Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha kimataifa cha China CGTN Bibi Liu Xin na mtangazaji kutoka channeli ya kibiashara ya Marekani Fox News Bibi Trish Regan wamefanya mazungumzo kuhusu mikwaruzano ya kibiashara kati ya China na Marekani kupitia kipindi cha moja kwa moja cha Fox News.

    Katika mazungumzo hayo, Bi Liu amezungumzia biashara kati ya China na Marekani, na pia hakimiliki za ujuzi.

    Bi Trish alimuuliza Bi Liu kama anaweza kueleza maoni yake binafsi kuhusu mjadala wa kibiashara kati ya China na Marekani. Bi Liu alijibu kuwa halifahamu jambo hilo kwa undani wake, hivyo hafahamu mjadala kati ya China na Marekani umefikia hatua gani, lakini anaona serikali ya China imeweka bayana msimamo wake.

    Wakati akizungumzia suala la hakimiliki ya ujuzi, Bi Liu amesema, kama pande mbili zikiweza kufundishana na kunufaishana, hakuna shida yoyote kwa upande mmoja kulipia hakimiliki za juzi za upande mwingine.

    Kuhusu hoja ya watu kuhofia maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini China, Bi Liu amesema, China imejiendeleza kama mtu anavyokua. Amesema kwa Wachina, hawapendi kuona China inakuwa nchi dhaifu siku zote, wanataka kuwa na nguvu kubwa zaidi. Lengo halisi ni jinsi nchi nyingine zinavyozichukulia nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako