• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ziara ya rais wa China nchini Russia kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo

  (GMT+08:00) 2019-05-30 16:34:10

  Rais Xi Jinping wa China atafanya ziara rasmi nchini Russia kuanzia tarehe 5 hadi 7 mwezi ujao, ambapo anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la 23 la St. Petersburg la Uchumi wa Dunia. Wizara ya mambo ya nje ya China imesema ziara hiyo itafungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Naibu waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Zhang Hanhui leo alipokutana na waandishi wa habari amesema, mabadiliko makubwa yanatokea duniani, wakati dunia inapokabiliwa na matishio ya ongezeko la vitendo vya upande mmoja na umwamba, uhusiano kati ya China na Russia umedumisha utulivu na maendeleo mazuri. Anasema,

  "Pande hizi mbili zinaaminiana kwa dhati katika mambo ya kisiasa, na kuungana mkono katika masuala makubwa yanayohusisha maslahi yao na kufuatiliwa nao kwa pamoja. Pia zimechangia utulivu wa hali ya kimataifa kwa kulinda mfumo na utaratibu wa kimataifa, pamoja na amani, utulivu, usawa na haki duniani."

  Bw. Zhang amesema katika ziara hiyo, rais Xi pamoja na rais Vladimir Putin wa Russia watafanya shughuli mbalimbali, ikiwemo kuhudhuria mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, kusaini makubaliano mawili ya ushirikiano wa kisiasa, na kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano kadhaa ya ushirikiano katika sekta nyingine. Bw. Zhang anasema,

  "Kupitia ziara hiyo, kwanza, viongozi wa nchi hizo mbili watatathmini uzoefu wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo katika miaka 70 iliyopita, na kutoa mpango wa kimkakati wa maendeleo ya uhusiano huo katika siku zijazo; pili, wataimarisha msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kuhakikisha uhusiano huo hauathiriwi na mabadiliko ya hali ya kimataifa; na tatu, wataanzisha mustakabali mpya wa ushirikiano wa nchi hizo katika sekta mbalimbali, ili kunufaisha zaidi watu na kuhimiza maendeleo ya nchi."

  Licha ya kufanya ziara rasmi nchini Russia, rais Xi pia atahudhuria Kongamano la 23 la St. Petersburg la Uchumi wa Dunia, na kutoa hotuba ya kutetea utaratibu wa pande nyingi, kukamilisha mfumo wa uendeshaji wa mambo ya kimataifa, na kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja wa dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako