• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwongo wa Pompeo kuongeza kasi ya kudhoofika kwa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-05-30 20:12:14

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo jana alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, Kampuni ya Huawei ni tishio kubwa zaidi kwa uchumi na usalama wa Marekani.

    Kufuatia mawazo ya Bw. Pompeo Marekani inaweza kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kuweka vikwazo dhidi ya makampuni ya nchi nyingine kwa kisingizio cha usalama. Bw. Pompeo anaona kuwa teknolojia ya 5G ni msingi wa usalama wa Marekani. Lakini Huawei peke yake inamiliki asilimia 20 ya hataza za teknolojia hiyo, huku makampuni yote ya Marekani yakiwa na chini ya asilimia 15 tu. Hivyo Marekani imeweka vikwazo dhidi ya Huawei kwa lengo la kuiangamiza.

    Je, Huawei ambayo ni kampuni binafsi ya China inaweza kuwa tishio la kwanza la usalama wa Marekani, ambayo ni nchi yenye nguvu zaidi duniani? Kauli hiyo inashangaza na kuchekesha. Tishio kweli kwa usalama wa dunia, ni kwamba Marekani inatumia ovyo nguvu yake.

    Marekani imeipaka matope kampuni ya Huawei mara nyingi, huku ikishindwa kutoa ushahidi halisi. Baadhi ya nchi zikiwemo Uingereza, New Zealand zimekataa kudanganywa na Marekani, kwani zimekagua vifaa vya Huawei kwa makini, na hazikugundua makosa yoyote.

    Shirika la habari la Bloomberg limetoa ripoti ikisema, Marekani "itajichoma moto" kwa kuweka vikwazo dhidi ya makampuni ya China. Makampuni makubwa ya teknolojia ya Marekani yakiwemo Microsoft na GE, yana wasiwasi kuwa uwezo wao wa ushindani utapungua kutokana na vikwazo hivyo. Uwongo wa baadhi ya wanasiasa wa Marekani akiwemo Bw. Pompeo hauwezi kuifanya nchi hiyo iwe na nguvu zaidi. Badala yake, utaongeza kasi ya kudhoofika kwa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako