• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Tuzo za Mo, Kagere, Mwamba wa Lusaka, Kotei, Manula, Nyoni wafunika

  (GMT+08:00) 2019-05-31 09:22:12

  Nyota wa kimataifa toka Rwanda anayekipiga klabu ya Simba ya Tanzania, Meddie Kagere ameendelea kudhihirisha kuwa, yeye ni moto wa kuotea mbali baada ya jana kutwaa tuzo mbili ya mchezaji na mshambuliaji bora wa mwaka kwenye hafla ya tuzo za Mo Simba mwaka huu.

  Tuzo ya kipa bora imeenda kwa Aishi Manula, huku beki bora amepata Erasto Nyoni amepata tuzo mbili, beki bora na mchezaji bora. Tuzo ya kiungo bora imenyakuliwa na James Kotei raia wa Ghana, huku Chama ameshinda tuzo mbili ya goli bora aliloifunga Nkana Red Devils ya Zambia latika hatua ya 32 bora ligi ya mabingwa Afrika. Rashid Juma amenyakua tuzo ya mchezaji bora chipukizi, kwa upande wa wanawake, Mwanahamisi Omary Shaluwa ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike, huku mfadhili wa zamani wa klabu hiyo Azim Dewji akinyakua tuzo ya heshima baada ya kuiwezesha klabu hiyo kufika fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika mwaka 1993.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako