• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Alama ya PMI nchini China kwa mwezi Mei yashuka

  (GMT+08:00) 2019-05-31 18:54:23

  Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, alama ya usimamizi wa manunuzi PMI nchini China kwa mwezi Mei imeshuka na kuwa asilimia 49.4, lakini uchumi wa China bado umedumisha maendeleo tulivu.

  Alama ya usimamizi wa manunuzi PMI nchini China kwa mwezi Mei ni asilimia 49.4, na kupungua kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na mwezi uliopita. Naibu mkuu wa Shirikisho la Uchukuzi na Uagizaji Bidhaa la China Bw. Cai Jin anaona kuwa, kushuka kwa PMI kunatokana na kuanza kwa majira ya mvua na kupungua kwa oda za nchi za nje. Anasema,

  "Kwanza ni sababu ya nje, oda mpya za nchi za nje zimepungua kwa kiasi kikubwa, na kuathiri kiwango cha PMI. Pili ni sababu ya majira, majira ya mvua yameanza katika baadhi ya sehemu za kusini nchini China, na imeathiri shughuli za ujenzi na uzalishaji."

  Wataalamu wanaona kuwa, kwa jumla uchumi wa China bado umedumisha maendeleo tulivu, kwani shughuli za uzalishaji na uagizaji wa bidhaa za teknolojia za juu bado zimeongezeka, huku sekta nyingi za viwanda zikikua. Takwimu zinaonesha kuwa, kati ya sekta 21 zilizochunguzwa za uzalishaji, sekta 19 zimepata maendeleo, haswa alama za ustawi wa sekta za utengenezaji upya wa mazao, vyakula, pombe, dawa, vifaa maalumu, reli, meli na mitambo zimezidi asilimia 58. Mbali na hayo, alama ya ustawi wa sekta zisizo za uzalishaji imezidi asilimia 54. Mshauri mkuu wa uwekezaji wa Shirika la Hisa la Guorong Bw. Yu Yao anasema,

  "Baadhi ya sekta zinazohusisha matumizi ikiwemo vyakula, vinywaji na dawa bado zinakua. Hivi sasa kwa jumla uchumi wa China una nguvu kubwa ya kukua. Hivyo tunaona kuwa matumizi yatachangia zaidi maendeleo ya uchumi katika siku zijazo."

  Takwimu pia zinaonesha kuwa, katika mwezi Mei, sekta ya huduma haswa uchukuzi wa reli na ndege, posta, hoteli, upashanaji habari, na software za mtandao, imedumisha ongezeko la kasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako