• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalipiza kisasi Marekani kama ilivyotamka

    (GMT+08:00) 2019-05-31 20:25:02

    Wizara ya biashara ya China leo imetangaza kuwa, kufuatia sheria husika, China itaanzisha orodha ya makampuni yasiyoaminika, ikiwa ni pamoja na makampuni yasiyofuata kanuni za kisoko, kukiuka mikataba, kukataa kutoa bidhaa kwa China bila ya malengo ya kibiashara, na kuathiri maslahi halali ya makampuni ya China.

    Hii ni hatua ya kulipiza kisasi kwa Marekani, ambayo imeweka vikwazo dhidi ya makampuni kadhaa ya China bila ya ushahidi wa makosa. China imefafanua kuwa haipendi na wala haiogopi vita vya kibiashara kati yake na Marekani. Katika zaidi ya mwaka mmoja uliopita, China imefanya duru 11 za mazungumzo na Marekani kuhusu suala la biashara. Wakati huohuo Marekani imeongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China mara kadhaa, na kuweka vikwazo dhidi ya baadhi ya makampuni ya China.

    Hali hii imeilazimisha China itoe majibu thabiti. Kuanzia tarehe mosi Juni, China itaongeza ushuru wa bidhaa kutoka Marekani kwa asilimia 25, 20 na 10, na kuanzisha orodha ya makampuni yasiyoaminika. Aidha China inafikiria kuuzuia utoaji wa udongo adimu kwa Marekani. Rais wa zamani wa Marekani Bw. Jimmy Carter alisema, Marekani ni nchi inayopenda vita zaidi duniani, lakini China haitumii pesa hata senti moja katika vita. Kweli China ni nchi inayopenda amani, na kuzingatia maendeleo. Inajua hakuna mshindi anayeweza kupatikana kutokana na vita ya kibiashara. Lakini Marekani imeilazimisha China kutoa majibu ili kulinda maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na dunia nzima, na mfumo wa kimataifa wa biashara ya pande nyingi.

    Hata hivyo, China inataka Marekani ifahamu vizuri kuwa, kuongeza ushuru wa orodha hakulingani na maslahi ya China wala Marekani, kuweka vikwazo dhidi ya makampuni ya China kutaathiri maendeleo ya sayansi na teknolojia, na ushirikiano ni njia sahihi pekee kwa China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako