• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa Mamlaka ya Posta ya China: Kampuni za nchi za nje zinazofanya biashara nchini China lazima zifuate sheria za China

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:03:50

    Kutokana na matukio ya kampuni ya FedEx ya Marekani kutopeleka vifurushi kwenye anuani za China, mkurugenzi wa mamlaka ya posta ya China Bw. Ma Junsheng amesisitiza kuwa, kampuni yoyote inayofanya biashara nchini China lazima ifuate sheria na taratibu za China, wala isidhuru maslahi halali ya kampuni na wateja wa China.

    Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mamlaka ya posta ilipokea malalamiko ya mteja dhidi ya kampuni ya FedEx ya Marekani, kwamba bila ya ruhusa ya mteja wala kumwarifu mapema, FedEx ilijiamulia kutuma vifurushi vya mteja hadi kwenye anuani nyingine. Bw. Ma amesema, kutofikisha vifurushi kwenye anuani iliyoambiwa na mteja ni kitendo kinachokiuka sheria husika za posta nchini China, pia kinadhuru maslahi halali ya mteja. Ndiyo maana mamlaka ya posta ya China imeamua kufanya uchunguzi kuhusu matukio hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako