• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema serikali ya Marekani inabeba lawama juu ya kukwama kwa mazungumzo ya kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:47:07

    China imesema shutuma zinazotolewa na serikali ya Marekani kuhusu China "kushindwa kufuata ahadi yake" katika mazungumzo hazina msingi hata kidogo, na inapinga kithabiti hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China na inatakiwa kuchukua hatua za lazima kujibu.

    Kwenye waraka uliotolewa leo na serikali ya China kuhusu msimamo wa China katika mazungumzo ya kibiashara kati yake na Marekani, China imesema makubaliano ya kibiashara yanatakiwa kuwa ya usawa na kusaidiana, na China haitarudi nyuma katika masuala makuu ya kimsingi yanayohusu maslahi makuu ya China. China imesisitiza kuwa sharti la kwanza kwa pande hizo mbili kufikia makubaliano, ni Marekani ifute ushuru wote za nyongeza, manunuzi yanapaswa kulingana na hali halisi, pia uwiano wa maudhui ya makubaliano unatakiwa kuhakikishwa na kulingana na maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako