• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China kunadhuru maslahi yake na ya wengine

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:50:03

    Waraka uliotolewa leo kuhusu msimamo wa China katika mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani umesema serikali ya Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China zinazoingia nchini Marekani kunazuia ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, na pia kunaathiri imani ya masoko ya nchi hizo mbili na ya kimataifa, pamoja na utulivu wa ukuaji wa uchumi.

    Waraka huo umeeleza kuwa hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu, thamani ya uuzaji bidhaa za China kwa Marekani ilikuwa imeshuka kwa miezi mitano mfululizo huku thamani ya uuzaji bidhaa za Marekani nchini China ikiwa imeshuka kwa miezi minane mfululizo. Sintofahamu zinazosababishwa na mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, zimezifanya kampuni za nchi hizo mbili ziwe na msimamo wa kusubiri na kuangalia uwekezaji na ushirikiano, uwekezaji wa China kwa Marekani umeendelea kupungua, na kasi ya ongezeko la uwekezaji wa Marekani nchini China pia imeshuka. Shirika la Biashara Duniani limepunguza makadirio ya kasi ya ongezeko la biashara ya dunia kutoka asilimia 3.7 hadi asilimia 2.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako