• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Joshua achezea kipigo raundi ya 7, haamini kilichotokea licha ya majigambo

  (GMT+08:00) 2019-06-03 08:08:54

  Bondia Muingereza Anthony Joshua amekula mweleka baada ya kukubali kichapo toka kwa mpinzani wake mmarekani mwenye asili ya Mexico Andy Ruiz alfajiri ya jana katika ukumbi wa Madison Square jijini New York Marekani kwenye pambano la uzito wa juu.

  Joshua amevuliwa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu baada ya kupigwa kwa Technical Knock Out (TKO) raundi ya saba ya mchezo huo.

  Ruiz hakuwahi kuangushwa kabla, lakini jana aliangushwa raundi ya tatu, kabla ya kuinuka na kuendelea na pambano. Joshua mwenye urefu wa futi sita atajaribu kurejesha mataji yake ya IBF, WBO na WBA katika pambano la marudiano mwezi Novemba mwaka huu. Hili ni pambano la kwanza Joshua kupoteza baada ya kushinda mapambano yote 22 ya awali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako