• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mambo matatu ya ukweli kuhusu mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-06-03 08:46:29

    Jumapili iliyopita serikali ya China ilitoa waraka rasmi kuhusu msimamo wa China kwenye mazungumzo ya kibiashara kati yake na Marekani, ambao umeweka bayana mambo ya ukweli kuhusu mgogoro wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, na vitendo vya Marekani vya kutokuwa na uaminifu kwenye mazungumzo hayo.

    Katika mwaka mmoja uliopita, China na Marekani zimefanya duru 11 za mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu masuala ya uchumi na biashara, na ziliwahi kupata maendeleo halisi kwenye mazungumzo hayo. Lakini Marekani haikuwa na msimamo, kwani iliendelea kuongeza ushuru mara kadhaa dhidi ya China, na kuibebesha China lawama za kusababisha kushindikana kwa mazungumzo hayo. Madhumini yake ni kuongeza zaidi shinikizo dhidi ya China, kujitafutia maslahi makubwa zaidi na kuidanganya jumuiya ya kimataifa.

    Ili kulinda maslahi ya watu wa China na haki yake ya kukuza uchumi, kwenye mazungumzo hayo China siku zote imejizuia kwa mantiki, lakini haimaanishi kuwa inaweza kukubali "ukandamizaji na upotoshaji" wa Marekani. Waraka huo wa kiserikali unalenga kuionesha dunia hali halisi ya mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani, na kusisitiza tena dhamira ya China ya kutorudi nyuma kwenye masuala makuu, na kuwataka wale wanaopenda ukandamizaji waache njonzi zao mapema.

    Mambo tatu ya ukweli yaliyofafanuliwa kwenye waraka huo ni yafuatayo:

    Kwanza, kukwama kwa mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani kunatokana na Marekani kutokuwa na msimamo. Marekani iliilaumu China kwa "kurudisha nyuma" msimamo wake, kwa lengo la kuibebesha China lawama za kushindikana kwa mazungumzo hayo na kutafauta kisingizio cha kuongeza ushuru dhidi ya China. Waraka huo umeweka bayana kuwa, Marekani kushikilia masharti yasiyowezekana, kushikilia kutofuta ushuru dhidi ya China, na kushikilia kuweka matakwa yanayoihujumu mamlaka ya China kwenye makubaliano, ndio chanzo cha kukwamisha mazungumzo hayo.

    Pili, maendeleo ya sayansi na teknolojia ya China yanatokana na uchapakazi na bidii, na wala sio wizi. Waraka huo umenukuu takwimu nyingi hasa zile zilizotolewa na mashirikisho ya viwanda na magezeti ya Marekani, na kuthibitha wazi kuwa lawama za Marekani hazina msingi wowote, na hatua za Marekani kutoza ushuru na kudhibiti uwekezaji dhidi ya China ni za umwamba.

    Tatu, kutoza ushuru dhidi ya nchi nyingine kunaharibu maslahi ya pande zote. Waraka umenukuu takwimu za utafiti zilizotolewa na taasisi za Marekani na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, na kuthibitisha kuwa hatua za kuongeza ushuru zimepandisha bei ya bidhaa nchini Marekani na kuathiri ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo na maisha ya wananchi wake, na pia zimetoa changamoto kubwa kwa ufufukaji wa uchumi wa dunia.

    Waraka huo pia umesisitiza tena msimamo thabiti wa China, kuwa kamwe haitarudi nyuma kwenye masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya taifa, na msingi wa kufikia makubaliano yoyote ni kuheshimiana, kunufaishana, usawa na uaminifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako