• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafafanua tena msimamo wake wa kufanya mazungumzo ya biashara na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-06-03 17:20:13

    Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China imetoa Waraka wa msimamo wa China kuhusu mazungumzo ya biashara kati yake na Marekani. Hii ni mara nyingine kwa China kutoa waraka kuhusu suala la biashara kati ya pande hizo mbili tokea mwezi Septemba mwaka jana. Wataalamu wanaona kuwa, waraka huu umefafanua kwa mara nyingine tena msimamo wa China wa kufanya mazungumzo kwa kufuata kanuni za usawa, kunufaishana, na kuaminika.

    Waraka huo umeeleza chanzo cha mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani, na hali ya kimsingi ya mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili, ukifafanua msimamo wa serikali ya China kuhusu mazungumzo hayo.

    Waraka huo umeeleza kuwa, uhusiano wa biashara kati ya China na Marekani ni injini ya kusukuma mbele uhusiano kati ya pande hizo mbili, na unahusiana na maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizo mbili, pamoja na ustawi na utulivu wa dunia. Tokea mwezi Machi mwaka 2018, ili kukabiliana na mgogoro wa biashara ulioanzishwa na Marekani, China ililazimika kuchukua hatua zenye nguvu ili kulinda maslahi ya nchi na watu wake. Wakati huo huo, imekuwa ikishikilia msimamo wa kutatua mgogoro huo kwa njia ya majadiliano, na kufanya duru kadhaa za mazungumzo na Marekani ili kutuliza uhusiano wa kibiashara kati ya pande hizo mbili.

    Mwenyekiti wa pamoja wa Kituo cha utafiti wa uchumi wa kimkakati cha China, Marekani na Ulaya kwenye Taasisi ya biashara ya kimataifa ya China Bw. Li Yong anaona kuwa, waraka huo uliotolewa na China umefafanua kwa mara nyingine tena msimamo wa China, kwamba China haitaki vita ya biashara lakini haitaogopa ya kuifanya kama ikilazimika. Bw. Li Yong anasema:

    "Tumeonesha hali halisi kwenye waraka huo, ambayo inalenga kufafanua ukweli wa mambo wakati Marekani itakapochukua hatua mbalimbali za mapambano, wakati huo huo tumeonesha msimamo kwa mara nyingine tena kwamba, China haitaogopa kufanya vita ya biashara kama ikilazimika, huku tukifungua mlango kwa kufanya mazungumzo."

    Waraka huo pia umeeleza kuwa, China siku zote inashikila msimamo wa kufanya mazungumzo kwa kufuata kanuni za usawa, kunufaishana na kuaminiana. Serikali ya China inaona kuwa vitendo vya kutoa tishio kwa kufanya vita ya biashara, na kuongeza ushuru kwa bidhaa za China havitasaidia utatuzi wa masuala ya kibiashara. Mkurugenzi wa Ofisi ya biashara ya kimataifa ya Idara ya mambo ya siasa na uchumi ya dunia kwenye Taasisi ya sayansi ya kijamii ya China Dong Yan anasema:

    "Waraka huo umeweka bayaba ujanja uliofanywa na Marekani katika mazungumzo ya biashara, na pia umeeleza wazi maslahi kuu ya China, huku ukionesha ishara wazi kwamba China inapenda kufanya mazungumzo kwenye msingi wa usawa, kunufaishana na kuaminiana. Lakini ushirikiano unapaswa kufanyika kwa kufuata kanuni, na China haitasalimu amri kwenye masuala muhimu, na itashikilia hatua ya mageuzi na ufunguaji mlango, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa njia ya kujiendeleza."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako