• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania inatafuta wawekezaji katika usindikaji wa njugu

    (GMT+08:00) 2019-06-03 20:01:42
    Tanzania inatafuta wawekezaji katika usindikaji wa njugu, kwa lengo la kuongeza matumizi ya ndani na kupunguza mauzo ya nje.

    Taasisi ya Uwekezaji Tanzania (TIC) imeandaa jukwaa mwezi ujao ambao lengo lake kuu ni kuvutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa katika sekta ya njugu, ambayo ina ukuaji wa wastani wa asilimia 450 kila mwaka.

    Geoffrey Mwambe, mkurugenzi mtendaji wa TIC anasema wanajaribu kuanzisha miradi ya usindikaji wa njugu na viwanda hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

    Usakaji wa wasindikaji unakuja wakati ambapo serikali ya Tanzania bado inashikilia idadi kubwa ya njugu ambayo kadiriwa kuwa tani 200,000 iliyonunuliwa kutoka kwa wakulima mwezi Novemba mwaka jana baada ya kushindwa kupata wanunuzi wa kigeni.

    Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa dunia wa karanga baada ya jumla ya uzalishaji kufikia tani 313,826 mwaka wa mazao wa 2017/18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako