• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Timu Samatta yatoa dozi kwa timu Alikiba, mechi ya mastaa kusaidia jamii

    (GMT+08:00) 2019-06-04 07:54:46
    Baada ya tambo za wiki nzima hatimaye mshindi amejulikana, nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambaye pia ni mchezaji wa timu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji amezungumzia ushindi waliopata kwa upande wa timu yake katika mechi ya Nifuate iliyoshirikisha timu Samatta na timu Kiba.

    Mechi hiyo ilikutanisha nyota wa mpira wa miguu wa Afrika mashariki akiwemo Jerry Santo wa Kenya, Meddie Kagere na Haruna Niyonzima wa Rwanda, Emmanuel Okwi wa Uganda na wengine wa Tanzania, iliandaliwa na Mbwana Samatta kushirikiana na msanii wa muziki nchini humo Ali Kiba.

    Mchezo huo ulioteka hisia za watu wengi ni moja ya mradi wa kusaidia jamii wa taasisi ya SamaKiba inayoundwa na Mbwana Samatta na Ali Kiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako