• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa UM ashtushwa na vikosi vya usalama vya Sudan kufyatua risasi ndani ya vituo vya matibabu

    (GMT+08:00) 2019-06-04 09:45:12

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani kitendo cha vikosi vya usalama vya Sudan kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.

    Msemaji wa katibu mkuu huyo Bw. Stephane Dujarric amesema, Bw. Guterres amefuatilia mashambulizi ya vikosi hivyo yaliyosababisha vifo na majeruhi ya watu wengi, na kueleza wasiwasi wake juu ya ripoti za askari hao kufyatua risasi ndani ya vituo vya matibabu.

    Wakati huo huo, msemaji wa Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan, Bw. Shams-Eddin Kabashi amekanusha ripoti juu ya kutawanywa kwa waandamanaji katikati mwa Khartoum.

    Habari nyingine zinasema, mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat pia amelaani vikali mashambulizi hayo.

    Katika siku za hivi karibuni, mji kuu wa Sudan, Khartoum, umeshuhudia matukio ya usalama karibu na makao makuu ya jeshi, ambako maelfu ya waandamanaji wameketi huko tangu tarehe 6, Aprili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako