• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kukabiliana kwa pamoja changamoto za mazingira

    (GMT+08:00) 2019-06-04 18:26:11

    Mkutano wa mwaka 2019 wa Kamati ya ushirikiano wa kimataifa kuhusu mazingira na maendeleo ya China unafanyika mjini Hangzhou, China. Waziri wa ikolojia na mazingira ya China Bw. Li Ganjie ameeleza kuwa, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kukabiliana na changamoto za mazingira duniani.

    Wataalamu 500 kutoka ndani nan je ya China wanaohudhuria mkutano huo wa siku mbili, wametoa mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira kwa China na nchi nyingine duniani.

    Waziri wa ikolojia na mazingira wa China Bw. Li Ganjie ameeleza kuwa, katika mwaka uliopita, China imeshiriki kwa kina katika mambo ya usimamizi wa mazingira duniani, na katika mwaka huu, itaendelea na ushirikiano huo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali duniani. Akisema:

    "China ikiwa nchi mwenyeji itatekeleza kwa pande zote majukumu yake, na kuandaa mkutano wa 15 wa pande zilizosaini 'Makubaliano ya viumbe anuai' utakaofanyika mwaka 2020, na kujadiliana na pande zote zilizosaini makubaliano hayo kuhusu waraka wa kimfumo wa viumbe anuai duniani baada ya mwaka 2020. Pia kutekeleza kwa kina mikakati ya taifa kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuendelea kushiriki kwenye mazungumzo ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kwa msimamo wa kiujenzi, kuzidi kusukuma mbele ushirikiano wa Kusini-Kusini katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kushirikiana na pande mbalimbali kutekeleza kwa makini makubaliano ya Paris, na kuhimiza Mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa wa mwaka 2019 kupata mafanikio."

    Mjumbe maalumu wa masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa wa China Bw. Xie Zhenhua ameeleza kuwa, katika miaka 20 iliyopita, kazi ya China katika jukwaa la mambo ya usimamizi wa mazingira ya dunia na maendeleo endelevu imepata mabadiliko makubwa, na China imebadilika kutoka kuwa mshiriki wa hatua ya mwanzo hadi mshiriki wa kina hivi sasa, na pia inajitahidi kuwa mwongozaji wa usimamizi wa hali ya hewa duniani katika siku za baadaye. Bw. Xie anasema:

    "China imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuweka lengo la utoaji wa hewa ya Kaboni kufikia kiwango cha kilele hadi kufikia mwaka 2030, ambayo ni ahadi ya China kwa jumuiya ya kimataifa, vilevile ni hatua ya kimkakati ya kupunguza utoaji wa hewa hiyo."

    Mshauri mwandamizi wa Taasisi ya rasilimali ya dunia Bw. Erik Solheim ameeleza kuwa, China inafanya juhudi ya kuongoza dunia katika mchakato wa ulinzi wa mazingira. Anatumaini kuwa China itaeneza uzoefu huo mzuri kwa dunia. Anasema:

    "Katika mwezi uliopita nimeshuhudia kuanzishwa kwa Shirikisho la kimataifa la maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', ambalo ni jukwaa zuri kwa kueneza uzoefu bora wa China katika sehemu nyingine duniani. Wakati huo huo tutaweza kutunga miongozo kwa kutumia fursa hiyo, na kutafuta njia bora ya maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako