• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawili wauawa kwenye mapambano kati ya vikosi vya Kenya na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab

    (GMT+08:00) 2019-06-04 19:18:48

    Watu wawili wameuawa na idadi nyingine ya wasiojulikana wamejeruhiwa kwenye mapambano kati ya vikosi vya usalama vya Kenya na wapiganaji wa Somalia kwenye kaunti ya Mandera kaskazini mashariki mwaka Kenya.

    Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Mashariki Bw. Mohamed Birik amethibitisha kutokea kwa mapambano hayo, mpiganaji mmoja wa kundi la al-Shabaab na mwanausalama mmoja wa akiba wameuawa katika eneo la Dawaduba, Fino kwenye kaunti ya Mandera,

    Kwa mujibu wa mamlaka za huko, watu wenye silaha walivuka mpaka na kuingia Kenya na kuweka kambi ili kufanya mashambulizi kwenye maeneo yasiyojulikana.

    Mapambano hayo yalitokea usiku, na kulikuwa na wasiwasi kuhusu wahanga zaidi. Mamlaka zimesema zinaendelea na operesheni dhidi ya wapiganaji hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako