• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara walilia mashine za kutengeneza karatasi

    (GMT+08:00) 2019-06-04 19:54:01

    Wajasiriamali wadogo ambao kwa sasa wamejikita katika utengenezaji wa mifuko ya karatasi, kutokana na zuio la mifuko ya plastiki mkoani Arusha, wameliomba Shirika la Viwanda Vidogo (Sido), kuanza mchakato wa kuwatafutia mashine ndogo zitakazopatikana kwa gharama nafuu.

    Ombi hilo limetolewa jana katika mafunzo ya uboreshaji wa mifuko ya karatasi kwa mahitaji halisi ya soko iliyoandaliwa na shirika hilo katika Mkoa wa Arusha, baada ya serikali kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Juni Mosi, mwaka huu.

    Akizungumza katika mafunzo hayo, mmoja wa wajasiriamali hao, Neema Mollel, alisema malengo yao makubwa ni kuhakikisha Watanzania wenyewe wanakamata soko la mifuko, badala ya kutegemea wageni kama ilivyokuwa kwa mifuko ya plastiki.

    Mollel alisema kupitia aina mbalimbali ya mafunzo, wameanza uzalishaji wa kawaida kwa kutumia vifaa vidogo vinavyopatikana madukani na akatoa rai kwa Sido kuhakikisha inatafuta mashine kwa ajili ya wajasiriamali wadogo kuzalisha mifuko kwa ufanisi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako