• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mane, Messi watajwa kikosi bora UEFA

    (GMT+08:00) 2019-06-05 08:21:39
    Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limetaja kikosi bora cha mastaa 11 waliong'ara kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu wa 2018/19.

    UEFA ilitangaza mastaa hao 11 bora muda mfupi kabla ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Liverpool na Tottenham Hotspur iliyopigwa katika uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid.

    Straika wa Barcelona, Lionel Messi, ambaye amepachika mabao 12 kwenye michuano hiyo yumo katika kikosi hicho akiwa ametajwa kwenye safu ya ushambuliaji.

    Nae Sadio Mane, ambaye aliiongoza timu yake ya Liverpool kwenye mechi ya fainali dhidi ya Tottenham Hotspur, yumo pia kwenye orodha hiyo ya wachezaji bora. Liverpool ndio imetoa wachezaji wengi zaidi katika kikosi hicho ikiwa imetoa watano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako