• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuwasaidia Wasomali waliokimbia ukame

    (GMT+08:00) 2019-06-05 09:07:55

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeonya dhidi ya kuongezeka kwa Wasomali wanaokimbia maafa ya ukame nchini mwao ambako watu zaidi ya milioni 2 wanahitaji msaada wa chakula.

    Shirika hilo limetoa wito wa misaada ya dharura ya ziada ili kuwasaidia watu walioathiriwa na kukimbia maafa ya ukame nchini Somalia, ambapo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu milioni 5.4 wanakadiriwa kukabiliwa na uhaba wa chakula kuanzia Julai, na watu milioni 2.2 kati yao watahitaji msaada wa dharura.

    Aidha, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP na UNHCR pia limeonya dhidi ya kuongezeka kwa hatari ya kukithiri kwa baa la njaa na utapiamlo katika eneo la Afrika Mashariki, hasa nchini Somalia, kama kanda hiyo itaendelea kukumbwa na uhaba wa mvua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako