• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahojiwa na vyombo vya habari vya Russia kabla ya kwenda Russia kwa ziara ya kiserikali

    (GMT+08:00) 2019-06-05 09:40:11

    Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alihojiwa na vyombo vya habari vya Russia kabla ya kwenda Russia kwa ziara ya kiserikali na kuhudhuria baraza la 23 la uchumi la kimataifa la St. Petersburg.

    Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la TASS la Russia, Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na Russia umepata fursa mpya ya maendeleo, na nchi hizo mbili zina nia na uwezo wa kuhimiza uhusiano huo kuingia kipindi kipya chenye kiwango cha juu zaidi na maendeleo makubwa zaidi.

    Akiulizwa kuhusu maoni yake juu ya mustakabali wa uchumi wa China, rais Xi amesema tangu mwaka huu, uchumi wa China umeendelezwa vizuri na vigezo vikuu vya uchumi viko kwenye viwango vinavyofaa. Vilevile miundo ya uchumi wa China inaboreshwa, mtindo wa maendeleo unabadilika, ufanisi na ubora umeongezeka na mwelekeo mzuri wa ukuaji wa uchumi ni dhahiri. Amesema China ina mazingira, uwezo na nia ya kukabiliana na hatari na changamoto mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako