• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashirikiana na jumuiya ya kimataifa kuisaidia Afrika kulinda urithi wa dunia

    (GMT+08:00) 2019-06-05 17:15:31

    Mkutano wa Baraza la ujenzi wa uwezo na ushirikiano kati ya UNESCO, China na Afrika umefanyika kuanzia tarehe 3 hadi 4 mwezi huu kwenye makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO yaliyoko huko Paris. Wajumbe kutoka UNESCO, mashirika ya ushauri wa urithi ya dunia, maofisa kutoka serikali za China na nchi za Afrika, pamoja na wataalamu wameshiriki kwenyhe mkutano huo wenye kaulimbiu "Urithi wa dunia na maendeleo endelevu: China na Afrika zapeana uzoefu".

    Afrika ni bara lenye urithi anuai wa kiasili na kiutamaduni. Lakini kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo njia isiyo endelevu ya kujiendeleza, vita, matumizi ya nguvu na siasa kali, uwindaji haramu, njia zisizo mwafaka za usimamizi na mabadiliko ya hali ya hewa, uhifadhi wa urithi kwenye bara hilo unakabiliwa na changamoto kubwa. Mwenyekiti wa mkutano wa UNESCO ambaye pia ni balozi wa kudumu Morocco kwenye shirika hilo Bi. Zohour Alaoui anasema:

    "Kati ya orodha ya majina ya urithi ulioko hatarini ya kutoweka duniani, theluthi moja iko kwenye Bara la Afrika, kwa upande mwingine, idadi ya urithi wa bara la Afrika ulioorodheshwa kati ya urithi wa dunia inachukua asilimia 9 tu ya idadi ya jumla ya urithi huo. Hali ambayo imetoa tahadhari kuhusu changamoto zinazotukabili."

    China vilevile ina idadi kubwa ya urithi wa kiutamaduni na kiasili. Tokea mwaka 1985 ilipojiunga na Makubaliano ya urithi ya dunia, idadi ya urithi wa China ulioorodheshwa kati ya urithi wa dunia imefikia 53, na imepata uzoefu mzuri katika kutekeleza makubaliano iliyoyasaini. Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikijihusisha katika ushirikiano wa kimataifa, kuzidi kuinua kiwango chake cha kuhifadhi na kusimamia urithi wake wenyewe pamoja na ule wa nchi nyingine duniani. Na inatumaini kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuisaidia Afrika kukabiliana na changamoto zinazoikabili. Balozi wa kudumu wa China katika UNESCO Bw. Shen Yang anasema:

    "Rais Xi Jinping wa China alipokutana na katibu mkuu wa UNESCO Bibi Audrey Azoulay mwezi Julai mwaka 2018, alifikia makubaliano muhimu na shirika hilo kuhusu kufanya ushirikiano katika kuunga mkono maendeleo ya Afrika. Mwezi Septemba mwaka 2018, rais Xi alifikia maafikiano na viongozi wa nchi za Afrika pamoja na Umoja wa Afrika kuhusu utekelezaji wa mipango minane ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwezo. China inapenda kuimarisha ushirikiano na UNESCO na nchi za Afrika, kuhimiza mawasiliano na mafunzo kati ya China na Afirka katika sekta ya urithi wa dunia, ili kuisaidia itimize malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030."

    Katibu mkuu msaidizi wa utamaduni kwenye UNESCO akimwakilisha katibu mkuu wa shirika hilo Bibi Azoulay ameeleza matumaini ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kuboresha uhifadhi wa urithi wa Afrika ulioorodheshwa kwenye urithi wa dunia. Mwenyektii wa Idara ya utekelezaji ya UNESCO Bw. Byong-Hyun Lee vilevile amepongeza juhudi za China na Afrika katika kuimarisha ushirikiano wa kulinda kwa pamoja urithi wa dunia, akiona kuwa hii ni sehemu muhimu katika ushirikiano kati ya kusini na kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako