• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: CAF yafuta matokeo ya fainali ya klabu bingwa Afrika

  (GMT+08:00) 2019-06-06 08:12:16

  Shirikisho la soka Afrika (CAF) baada ya kukaa kikao cha dharula jijini Paris Ufaransa imetoka na majibu ya kufuta matokeo ya michezo yote miwili ya fainali ligi ya mabingwa Afrika kati ya Wydad Casablanca dhid ya Esperance.

  Kutokana kufutwa kwa matokeo hayo klabu ya Esperance ya Tunisia italazimika kurudisha kombe pamoja na medali za ubingwa za wachezaji wake walizokuwa wamepewa baada ya wachezaji wa Wydad kugoma kuendelea na mchezo.

  Mchezo huo wa fainali utachezwa baada ya fainali za AFCON, Esperance ilipewa ubingwa kufuatia wachezaji wa Wydad kugoma kuendelea na mchezo baada ya goli lao kukataliwa dakika ya 59 na muamuzi Bakary Gassama kutokea Gambia na kukataa kwenda kuangalia uhalali wa goli hilo kupitia VAR.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako